Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Ibrahim al-Sarraj, mchambuzi wa kisiasa kutoka Iraq, anaamini kuwa Iran imeibuka mshindi dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani, na imeweza kuuvunja na kuuangusha mpango wa "Mashariki ya Kati Mpya" wa Kiamerika-Kizayuni.
Al-Sirraj alisema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, licha ya vita na uvamizi wa Israel, Marekani na NATO, imepata ushindi mkubwa mno dhidi ya utawala wa Kizayuni, na imeweza kuthibitisha haki yake ya kuwa na nishati ya nyuklia."
Akaongeza kusema: "Iran vilevile imeweza kuthibitisha haki yake ya kuzakisha uraniam, kwa sababu maadui wake – licha ya kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran – hawakuweza kuuzuia mradi wake wa uzalishaji wa uraniam.
Mchambuzi huyo wa kisiasa kutoka Iraq alifafanua kuwa: Tehran haikusalimu amri mbele ya mashinikizo ya kisiasa na ya kijeshi ya kimataifa yaliyolenga kuilazimisha iachane na mpango wake wa makombora, na licha ya ukali wa vita na kampeni za vyombo vya habari vya kimataifa dhidi ya Iran, haikunyanyua bendera nyeupe mbele ya adui. Matokeo yake ni kuwa Iran imekuwa ngome ya ulinzi wa eneo hili, na imeuangusha mradi mpya wa “Mashariki ya Kati” wa Kiamerika-Kizayuni.
Maoni yako